Kundi la muziki tokea nchini Congo(D.R.C) yenye mji mkuu wake ukijulikana hapo zamani kama Léopoldville na sasa Kinshasa lilianzishwa mnamo mwaka 1981 wakikutana Didier Masela Aime Bwanga Werrason na Allen Mwanga kwa pamoja vijana hawa walifanya ubunifu mkubwa katika miondoko ya soukous na kuifanya soukous yakisasa zaidi na yainayake iliyowavutia sana vijana wa enzi hizo.Waimbaji wa kundi la Vivala Musica na Zaiko LangaLanga kama vile JB Mpiana Blaise Bula na Marie Paul walishawishika kujiunga na kundi hilo. Wakiwa wanarekodi "Kun E Bouge" katika jiji la Paris nchini Ufaransa Marie Paul aliamua kubaki ufaransa. Wakati Aime Bwanga na Alan Mwanga walianza kuwafua vijana nakuanzisha kundi lingine likiitwa Wenge Aile Paris. Hivyo kukawa na makundi mawili Wenge Aile Paris likibaki Paris Ufaransa na Wenge BCBG likibaki Congo Kinshasa likiwa na Werrason na JB Mpiana Kama viongozi. Wenge BCBG walifyatua album yao ya kwanza ikiitwa "Kin Bouge" ikifuata Kala Yi Boeng Utunzi wake Werrasson na nyingine nyingi kama vile Pentagone, Masampu na nyinginezo nyingi. Mnamo miaka ya 1996 na 1997 JB Mpiana aliamua kutoa Album yake binafsi ikiitwa ''Feux de lamour ''bila kushirikisha wenzie. Huo ndiyo mwanzo wa kusambalatika kwa kundi la Wenge BCBG. Mwaka 1997 December walitengana kabisa viongozi wa kudi hilo yaani Mpiana na Werrason. JB Mpiana alibaki na Jina la Wenge BCBG akiwa na wanamuzi kama Allan Makaba (Prince) Allan Mpera (Afande) Blaise Bula Aimelia, Ekokota,Tutu Calugi. Kwa upande wake Werrason alianzisha Wenge Musica Maison Mere akiwa na wanamuziki kama Adolphe Dominguez na Didier Masela. Unakaribishwa utoe mchango wako au uongeze chochote kitu kuhusiana na Wenge Muzica
asante kaka
ReplyDelete